Wednesday, August 22, 2012

TAZAMA FIESTA SUPA NYOTA ILIVYOFANA PALE SUN CIRO


Hawa ndio washindi wa Fiesta Supa nyota, kutoka kushoto ni Joh maker, Neily na Young Killer

Young Killer kutoka Mwanza  akiperform kwenye stage

Joh Maker akionyesha uwezo kwa mashabiki wake kwenye stage ya Sun Ciro

Neily kutoka mbeya naye akionyesha uwezo wake wa kuimba kwenye stage

Hawa ndio walikuwa Majudge wa shindano ili la Serengeti Fiesta Supa nyota 2012
Siku ya Jumapili wapenzi wa Muziki nchini waliweza kuwajua washindi wa Serengeti Fiesta Supa nyota 2012 baada ya fainali kufanyika pale club Sun Ciro sinza jijini Dar es Salaam.
Baada ya kupata wawakilishi wa mikoani nakuweza kuja hapa Dar es Salaam kwa ajili ya  fainali hizi za Supa Nyota na washiriki  hao walikuwa kama ifuatayo:- Jordan kutoka Dar, Young killer kutoka Mwanza, Rider kutoka Tanga, G 5 kutoka Arusha, Super J kutoka mbeya, Muya kutoka Dar, Joh maker kutoka Moro, T y kutoka Dar, Neily kutoka Mbeya, Master jay kutoka  Moro, Candy kutoka Dar. Baada ya kuanza mashindano  haya round ya pili tulifanikiwa kupata washiriki sita ambao washiriki hawa walipewa Dakika mbili za kuweza kukionyesha kile ambacho wanacho mpaka ma judge na mashabiki wao wakubali kile wanachokitoa hapo kwenye stage.
Baada ya washiriki wote kupewa dakika mbili za kuimba tulifanikiwa kupata Supa nyota watatu ambao ni Young Killer kutoka Mwanza, Joh Maker kutoka Moro na Neily kutoka Mbeya ammbao watazunguka mikoa  yote ambayo Serengeti  Fiesta 2012 itafanyika .

0 comments: